×

SKARAMENTI YA NDOA TAKATIFU


IBAADA YA PETE

KASISI

Ahimidiwe Mungu wetu, daima, sasa na siku zote, hata milele na milele.

(Amina.)

Kwa amani tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya amani ya dunia yote na kusimama imara kwa Ekklesia takatifu ya Mungu na kwa umoja wa wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya watumishi wa Mungu (Bwana Harusi) na (Bibi Harusi), ambao wanaunganishwa kwa Ndoa na kwa ajili ya wokovu wao, tumombe Bwana.

Ili washukiwe na upendo wa amani timilifu, na msaada wa Mungu, tumuombe Bwana.

Ili watunzwe na wabarikiwe na umoja wa fikira na imani timilifu, tumwombe Bwana.

Ili wadumishwe kwa mwenendo bora na maisha yasiyo na lawama, tumuombe Bwana.

Ili Bwana Mungu wetu awape ndoa yenye heshima isiyo na lawama, tumuombe Bwana.

Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sikitiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.

Utulinde, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi Ee Mungu kwa neema yako.

Tumkumbuke Maria mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, sisi wenyewe na wenzetu wote, hata maisha yetu, tujiweke mikononi mwa Kristo Mungu.

(Kwako, Ee Bwana.)

Kwa kuwa utukufu wote, heshima na usujudu ni haki yako, Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

(Amina.)

KASISI

Tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Ee Mungu wa milele, uliyefanya watu waliotengana kuwa na umoja, na ukaanzisha uelewano usiovunjika kwao; na ukawabariki Isaka na Rebeka na kuwafanya warithi wa hadi, yako: Wabariki hawa watumishi wako (jina) na (jina) na uwaongoze kwa kila kazi njema.

Kwa kuwa u Mungu mrahimu na mpenda-wanadamu na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.

(Amina.)

Amani kwa wote.

(Na iwe kwa roho yako.)

Tuinamishe vichwa vyetu mbele ya Bwana.

(Kwako, Ee Bwana.)

Ee Bwana Mungu wetu, unayelifanya Kanisa kuwa bikira asiye na ndoa toka kwa mataifa yote; ubariki pete hizi na uwaunganishe na uwahifadhi watumish (majina) wako, kwa amani na mapatano.

Kwa kuwa utukufu, heshima na usujudu ni haki yako Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

(Amina.)

Mtumishi wa Mungu (Jina) anatoa ahadi kumuoa mtumishi wa Mungu (Jina), kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. (Amina.) (x 3)

Mtumishi wa Mungu (jina) anaahidi kuolewa na mtumishi wa Mungu (Jina), kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. (Amina.) (x 3)

Tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Ee Bwana Mungu wetu, uliyeambatana na mtumishi wa Ibrahimu kwenda Mesopotamia, ambapo alikuwa ametumwa kumtafuta mchumba wa Isaka, kwenye kisima alichoonyeshwa kwamba ni sharti kumposa Rebeka kama mchumba. Bariki uchumba wa hawa watumishi wako (Majina), na imarisha ahadi ambazo wameahidiana kwa umoja wa utakatifu, kwa kuwa tangu mwanzo uliwaumba Mme na Mke, na kwa mapenzi yako Mke anaungana na Mme kusaidiana na kuendeleza ubinadamu. Ndiwe uliyetuma ukweli wako na urithi wako na ahadi yako kwa watumishi wa Baba zetu, na wateule wako kutoka kizazi hata kiazi, watunze hawa watumishi wako jina (majina) na uimarishe ndoa yao kwa imani, mapatano, ukweli na upendo; kwa kuwa wee Bwana ndiwe ulitufunza kufunga harusi kwa ahadi ya pete na kuaminiana kwa kila jambo. Kutokana na pete, Yusufu alipewa madaraka katika nchi ya Misiri. Kwa kutumia pete, Danieli alitukuzwa katika Babiloni; Damari alitambuliwa kuwa na haki, kutokana na pete. Baba yetu wa Mbinguni alionyesha huruma kwa Mwana mpotevu; akisema "Weka Pete kwenye kidole chake na umlete Dume aliyenona achinjwe ili tule na kushangilia. Ee Bwana mkono wa kuume ulimwenzesha Musa kuvuka bahari ya Sham, kwa maneno yako ya ukweli, mbingu zilimarishwa na nchi kubwa; uwambariki hawa waumishi wako kwa mkono wako wa kuume. Sasa Ee, Bwana kwa baraka za mbinguni, bariki kuvalishana huku na Pete. Malaika wa Bwana awe nao katika maisha yao yote.

Kwa kuwa wewe ndiwe unayebariki na kutakasa vitu vyote ; na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

(Amina.)


IBAADA YA TAJI

Zaburi ya 127 (128).

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu kwako.

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu kwako.

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu kwako.

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu kwako.

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu kwako.

KASISI

WATU

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu kwako.

KASISI

Mhimidiwa ni ufalme wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

(Amina.)

Kwa amani tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya amani ya dunia yote na kusimama imara kwa Ekklesia takatifu ya Mungu na kwa umoja wa wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya Papa na Patriarka wetu ..., Askofu wetu mkuu ..., [swh_ke_oak] [swh_ke_oak] makasisi waaminifu, mashemasi katika Kristo, wateule na watu wote, tumwombe Bwana.

Kwa ajili ya watumishi wa Mungu (majina) ambao wanaunganishwa kwa ndoa na kwa ajili ya wokovu wao, tumuombe Bwana.

Ili hii ndoa ibarikiwe kama iliyokuwepo Kana ya Galilaya, tumuombe Bwana.

Ili wapewe hukumu ya utu na watoto kwa manufaa yao, tumuombe Bwana.

Ili wajazwe kwa furaha wakiwaona wavulana na wasichana, tumuombe Bwana.

Ili wambarikiwe na watoto wema na maisha ya haki, tumuombe Bwana.

Ili Mungu apokee maombi ya wokovu wetu, tumuombe Bwana.

Ili sisi tukombolewe toka katika sikitiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumuombe Bwana.

Utulinde, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi Ee Mungu kwa neema yako.

Tumkumbuke Maria mtakatifu kamili, asiye na doa, mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu, Mzazi-Mungu na Bikira daima, pamoja na watakatifu wote, sisi wenyewe na wenzetu wote, hata maisha yetu, tujiweke mikononi mwa Kristo Mungu.

(Kwako, Ee Bwana.)

Kwa kuwa utukufu wote, heshima na usujudu ni haki yako, Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

(Amina.)

KASISI

Tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Ee Mungu usiye na doa, muumba wa vitu vyote kwa upendo wako kwa mwanadamu ulimuumba Eva kwa Ubavu wa babu yetu Adamu na ukawabariki ukisema " Zaeni makaongezeke mkaijze nchi na mkaitawale." nawe ukawafanya wote kuwa kitu kimoja kwa kuwaunganisha kwa hivyo Mme atawaacha Baba na mama na kuambatana na mke nao watakuwa mwili mmoja na yale ambayo umeunganisha, mwanadamu asiwatenganishe. Ulimpatia Sara kwa Ibrahimu na ukawabariki kuwapa mtoto na kumafanya Baba wa mataifa. Uliunganisha Isaka na Rebeka na ukawabariki kwa kuwapa mtoto, pia ulinganisha Yakobo na Recho na kwao mababu kumi na wawili wakazaliwa; uliwaunganisha Yosifu na Asenati na ukawapa Ephraim na Manasseh kama watoto wao, uliitikia Zacharia na Elizabeth na ukamfanya Mwana wao kuwa mtangulizi, na kwa uzao wa Jesee ilimteua Bikira Maria ambapo ulizawa ukiwa mtu asilikwa wokovu wa mwandamu, kwa neema yako isiyoelezeka na wema wako ulisafiri huko Kana ya Galilaya ukabariki harusi huko; kwa uzao wa watoto ni kwa mapenzi yako. Kwako Ee Bwana Mtakatifu wa wote; uyakubali maombi yetu na jinsi ulivyokuwa huko na pia uwe nasi hapa kwa kutoonekaana kwako.Ibariki ndoa hii na uwape watumishilifu wako (majina) maisha ya furaha miaka ming, hukumu timilifu mapenzi kati yao na umoja wa amani, maisha marefu, neema kwa watoto wao na taji ya utukufu wa milele - uwawezeshe kuwaona wajukuu wao. Dumisha ndoa yao isiabke na uwape baraka toka mbinguni na utajiri wa ulimwengu. Ijaze nyumba yao kwa ngano, divai na chote kilichochema, ili waweze kuwasaidia wale wanaohitaji. Na utustahilishe sisi tulioko hapa kwa maombi yanayotuongoza kwa wokovu.

Kwa kuwa wewe ni Mungu mwenye huruma na upendo na kwako tunatoa utukufu pamoja na Baba yako asiye na mwanzo pamoja na watakatifu wote, na Roho mwema mpaji wa uhai sasa na siku zote hata milele na milele.

(Amina.)

KASISI

Tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Uhimidiwe Ee Bwana Mungu wetu uliye mwidhinishaji wa ibada hii ya Ndoa (Sakramenti) takatifu, uliye mchungaji mwema wa zawadi ya maisha haya. Mwanzoni Ee Bwana uliumba mtu, ukamfanya kuwa kiongozi katika ulimwengu ukisema "Si vyema Mme kuwa peke yake, nitamfanya mzaidizi wa kufanana naye". Kwa kutoa ubavu wake mmoja ulimuumba Eva hapo Adamu alipomuona alisema,"Sasa huyu ni mfupa wangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametawaliwa na mwnaume ataawacha Baba na Mama na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwile mmoja na wale ambao wameunganishwa na Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Ee Bwana Mungu wetu, shukisha neema yako toka Mbinguni kwa hawa watumishi wako (majina). Fanya bibi harusi kuwa mtiifu kwa Mmewe, na huyu mtumishi ako awe kiongozi wa Mke, ili waishi kwa mapenzi yako. Wambariki Bwana Mungu wetu jinsi ulivyowabariki Abraham na Sara, Isaka na Rebeka, Yakobo na Recho nao wengine kama Yosefu na Asenati, Musa na Zipora, Yoakim na Anna, Zakaria na Elizabeth. Walinde kama vile ulivylimlinda Nuhu kwenya Safina, Yona tumboni mwa Nyangumi nao vijana watatu watakatifu toka motoni. Wabariki kwa baraka za mbinguni na uwajaze kwa furaha kuu kama ile iliyo mjaa Helena alipoupata Msalaba wenye dhamana. Wakumbuke kama ulivyowakumbuka Enoka Shem Eliya na pia mashahidi Arobaini waliyotunukia taji la mbinguni, uwakumbuke Ee Bwana Mungu, wazazi walio walea, kwa baraka zao wazazi imarisha msingi wa nyumba yao. Bwana Mungu watumishi wako wote walioko hapa wanao hudhuria ndoa hii. Wakumbuke Bwana ba Bibi arusi (majina) na uwabariki kwa uzao wa watoto wema, na miili na mioyo yao iwe kitu kimoja. Watukuze kama miche ya Lebanoni iliyo mizabibu ya kupendeza, waweze kuaona wajukuu wao miti mipya ya mizeituni iliyopandwa kuzingira meza yao. Waing''aishe kama nyota za mbinguni; kwako tunatoa utukufu, utawala, heshima na usujudu; ni haki yako sasa na siku zote hata milele na milele

(Amina.)

KASISI

Tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Mungu Mtakatifu uliye muumba mtu kwa udongo na Mwanamke kwa ubavu wake na kuwaunganisha kwake awe msaidizi wake. Kwa vile kulionekana kwamba Mme asiwe peke yake ulimwenguni, Nyoosha mkono wako toka kwenye makao yako matakatifu na uwaunganishe hawa watumishi wako (Majina) pamoja kwa ajili hiyo Mke ataungana na Mme. Waunganishe katika fikira moja, wavike taji ya pingu za maisha katika mwili mmoja; wajalie uzao wa tumbo, na kuwepo kwa watoto wsenye baraka.

Kwa kuwa ufalme na uwezo na utukufu ni wako, wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

(Amina.)

KASISI

Mtumishi wa Mungu (jina) anvikwa Taji na mtumishi wa Mungu (Jina), kwa jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu, (Amina.) (x 3)

Kwa kuwa utawala ni wako na ufalme na uweza na utukufu, ni wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. (Amina.) (x 3)

WATU

Wavike taji Ee Bwana Mungu wetu, kwa heshima na utukufu wako. x 3.

MASOMO

MSOMAJI

Zaburi

KASISI

Tusikilize.

MSOMAJI

KASISI

Hekima.

MSOMAJI

Somo katika Paul''s Letter to the Ephesians.

KASISI

Tusikilize.

MSOMAJI

5:20-33

Brethren, always for everything give thanks in the name of our Lord Jesus Christ to God the Father. Be subject to one another out of reverence for Christ. Wives, be subject to your husbands, as to the Lord. For the husband is the head of the wife as Christ is the head of the church, his body, and is himself its Savior. As the church is subject to Christ, so let wives be also subject in everything to their husbands. Husbands, love your wives, as Christ loved the church and gave himself up for her, that he might sanctify her, having cleansed her by the washing of water with the word, that he might present the church to himself in splendor, without spot or wrinkle or any such thing, that she might be holy and without blemish. Even so husbands should love their wives as their own bodies. He who loves his wife loves himself For no man ever hates his own flesh, but nourishes and cherishes it, as Christ does the church, because we are members of his body. "For this reason a man shall leave his father and his mother and shall be joined to his wife, and the two shall become one." This is a great mystery, and I take it to mean Christ and the church; however, let each one of you love his wife as himself, and let the wife see that she respects her husband. [RSV]

KASISI

Amani kwako Ee Msomaji.

WATU

Alleluya, Alleluya, Alleluya.

Mstari 1:

Alleluya, Alleluya, Alleluya.

Mstari 1:

Alleluya, Alleluya, Alleluya.

KASISI

Hekima. Simameni wima. Tusikilize Injili takatifu. Amani kwa wote.

(Na iwe kwa roho yako.)

Injili Takatifu kama ilivyoandikwa na John. Sura... mstari... Tusikilize.

(Utukufu kwako, Ee Bwana, Utukufu kwako.)

2:1-11

At that time there was a marriage at Cana in Galilee, and the mother of Jesus was there; Jesus also was invited to the marriage, with his disciples. When the wine failed, the mother of Jesus said to him, "They have no wine." And Jesus said to her, "O woman, what have you to do with me? My hour has not yet come." His mother said to the servants, "Do whatever he tells you." Now six stone jars were standing there, for the Jewish rites of purification, each holding twenty or thirty gallons. Jesus said to them, "Fill the jars with water." And they filled them up to the brim. He said to them, "Now draw some out, and take it to the steward of the feast." So they took it. When the steward of the feast tasted the water now become wine, and did not know where it came from (though the servants who had drawn the water knew), the steward of the feast called the bridegroom and said to him, "Every man serves the good wine first; and when men have drunk freely, then the poor wine; but you have kept the good wine until now." This, the first of his signs, Jesus did at Cana in Galilee, and manifested his glory; and his disciples believed in him.

(Utukufu kwako, Ee Bwana, Utukufu kwako.)

KASISI

Utuhurumie Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.

Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

Tena tunakuomba kwa ajili ya watumishi wa Mungu (Jina) na (Jina)- Ili wapate huruma, uzima, afya, amani, ulinzi, wokovu, maisha na maondoleo ya dhambi.

Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.

Kwa kuwa u Mungu mrahimu na mpenda-wanadamu na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.

(Amina.)

KASISI

Tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Ee Bwana Mungu wetu ulitoa wokovu na kuamuru ndoa ya heshima kwa kushiriki kwako Kana ya Galilaya; Waweke kwenye amani na mapatano hawa watumishi wako (Majina) ambao wamefurahia kuunganishwa kwa kwao pamoja. Ifanye ndoa yao kuwa yenye heshima, na uhifadhi, ili waweze kuishi pamoja bila hatia. Wape maisha marefu kwa kutimiza amri na moya mwema.

Kwa kuwa Wewe ni Mungu Mwenya huruma na Mwokozi wetu, na kwako tunatoa utukufu pamoja na Baba wako asiye na mwanzo, na Roho wako mtakatifu na mpaji wa uhai, Sasa na siku zote hata milele na milele.

(Amina.)

KASISI

Na utustahilishe, Ee Bwana wa mabwana tukiwa na uthabiti bila hukumu tuwe na ujasiri kukuita Baba uliye Mbinguni na kusema.

WATU

Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Na utusamehe deni zetu, kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu. Tena usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.

KASISI

Kwa kuwa ufalme na uweza na utukufu, ni wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.

(Amina.)

KUBARIKI KUPOKEA KIKOMBE CHA USHIRIKA.

KASISI

Tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Ee Mungu uliye umba vitu vyote kwa uwezo wako, ulimwengu tena ukarembesha vyote ulivyoumba. Bariki kikombe hiki cha ushirika kwa baraka zako takaktifu na kuwapatia wanaoungana katika ndoa.

Kwa kuwa jina lako limehimidiwa na ufalme wako unatukuzwa, Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.

(Amina.)

WATU

Wimbo wa Ushirika

Enyi mashahidi watakatifu wapiganaji wema ambao wamevikwa taji, mtuombee ili azihurumie roho zetu

Utukufu Kwako Ee Kristo Mungu wetu, Mitume Kristo wetu, mitume wasifiwa na wenye fahari na mashahidi wapendwa walio na ujumbe wa utatu mtakatifu.

KASISI

Ewe Bwana harusi utukuzwe kama Ibrahimu na ubarikiwe kama Isaka na uwe na uzao kama vile Yakobo: utembee kwa haki na utimize amri zake Mungu.

Nawa Bibi harusi , utukuzwe kama vile Sara na uwe na furaha kama Rebeka, uwe na uzao kama Recho ukishangilia katika Bwana wako, na kuzingatia wajibu wa sheria kwa kuwa Mungu amefurahia.

KUONDOLEWA TAJI VICHWANI:

KASISI

Tumwombe Bwana.

(Bwana, hurumia)

Ee Mungu, Mungu wetu aliye kwenda mjini Kana ya Galilaya na ukambariki ndoa huko, ubariki hawa watumishi wako, ambao kwa uwezo wako wameungana pamoja na jamii kwa ndoa, Bariki kwenda na kurejea kwao. Wafariji na maisha ya ut, vitu vyema chukua taji zao (* Anatoa taji vichwani mwao). Katika ufalme wako zikihifadhiwa bila kuharibika, kulaumiwa na kuambika hadi milele na milele.

(Amina.)

KASISI

Amani kwa wote.

(Na iwe kwa roho yako.)

Tuinamishe vichwa vyetu mbele ya Bwana.

(Kwako, Ee Bwana.)

MAOMBI KWA BWANA HARUSI NA BIBI HARUSI.

KASISI

Kwa uweza wa Mungu Baba, Mungu Mwana Roho Matakatifu, utatu mtakatifu usiotengana na ufalme wako, uwape watoto wazuri, maisha ya ufanisi, kukua katika imani na uwajaze na vitu vyote vyema vya ulimwenguni; Wafurhishe na wema wa baraka zilizoahidiwa kwetu. Kwa maombezi ya Maria Mtakatifu na watakatifu wote.

(Amina.)

TAMATI

KASISI

Utukufu kwako, Ee Mungu wetu, utukufu kwako.

Kristo Mungu wa ukweli ambaye kuja kwake Kana ya Gallaya na kufanya ndoa kuwa yenye heshima. Kwa maombi ya Maria Mzazi Mungu asiye na ndoa lo lote, mitume watukufu na wasifiwa na kwa wafalme watukufu na wasifiwa na Mungu sawa na mitume. Constantino na Hellen shahidi mtakatifu Prokopius na watakatifu wote utuhurumie na kutuokoa kwa kuwa yu Mungu mwema na mpenda wanadamu.

Kwa maombi ya mababa wetu watakatifu, Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, utuhurumie na utuokoe. Amina.

(Amina.)